Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Serikali ya Urusi mjini Moscow imependekeza hii leo kwamba Urusi na Marekani zianzishe operesheni za pamoja za jeshi la wanaanga dhidi ya wanamgambo wa makundi ya kigaidi nchini Syria - Al Nusra na makundi mengine ya kigaidi. Moscow inapendekeza operesheni hizo za pamoja zianze wiki inayokuja. "Tunapendekeza, Marekani ambayo ndiyo inayoongoza kundi la kimataifa la nchi shirika kwa ajili ya Syria ishiriki kuanzia Mei 25 katika operesheni za pamoja kati ya vikosi vya wanaanga wa Urusi na vikosi vya nchi shirika" amesema hayo waziri wa ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu kupitia televisheni ya nchi hiyo. Hadi wakati huu nchi hizo mbili zilikuwa zikiwaandama magaidi kila mmoja kwa upande wake.
Urusi inapambana dhidi ya makundi yote ya kigaidi ambayo yako Zaidi ya makundi 10 nchini Syria lakini Marekani na washirika wake wanapambana na makundi mawili tu na kuyaacha mengine ambayo wanayasaidia silaha ili kuiangusha serikali ya Syria.
Makubaliano ya amani yaliyofikiwa kutokana na juhudi za Urusi na Marekani yamesaidia kupunguza matumizi ya nguvu nchini Syria, hata hivyo yamekuwa mara kwa mara yanaendewa kinyume baada ya magaidi wanaodhaminiwa na Marekani na washirika wake.
Mwisho wa habari/ 291